Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 6:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 ilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hatta kudhihiri kwake Bwana wetu Yesu Kristo,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka siku ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 uishike amri hii bila dosari wala lawama hadi kufunuliwa kwake Bwana wetu Isa Al-Masihi;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 uishike amri hii bila dosari wala lawama mpaka kuja kwake Bwana wetu Isa Al-Masihi,

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 6:14
28 Marejeleo ya Msalaba  

na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.


apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;


mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima;


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;


Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,


illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo:


Maana ingekuwa kheri kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua ile amri takatifu waliyopewa na kuiacha.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo