Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 6:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, upendo, subira na unyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, upendo, subira na unyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, upendo, subira na unyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 6:11
40 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.


Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.


UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.


Ikimbieni zina. Killa dhambi aifanyayo mwana Adamu ni nje ya mwili wake; bali yeye afanyae zina hufanya dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.


na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.


Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;


Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema.


Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi.


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo