Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Timotheo 6:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

Tazama sura Nakili

1 Timotheo 6:10
49 Marejeleo ya Msalaba  

Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba:

na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.

Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:

si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha;

wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nawe.

Watakao kuwa na mali waanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa zisizo maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wana Adamu katika upotevu na uharibifu.

Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,

maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.

ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.

Ndugu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali ya kweli, na mtu mwingine akamrejeza;

Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.

na mdalasini, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na nganu, na ngʼombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wana Adamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo