Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 5:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Bali yeye aliye mjane kweli kweli, na kuachwa peke yake, amemwekea Mungu tumaini lake, nae hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mwenyezi Mungu, naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 5:5
27 Marejeleo ya Msalaba  

AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa,


Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.


nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana.


ambayo kabila zetu thenashara wanataraja kuifikia, wakimkhudumu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, ee Mfalme.


HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.


Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika wakampeleka juu orofani: wajane wote wakasimama karibu nae, wakilia na kuniwonyesha zile kanzu na nguo alizozifanya Paa wakati ule alipokuwa pamoja nao.


Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi.


yaani, tufarijiane mimi na ninyi, killa mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Lakini nataka inwe hamna masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;


Tena iko tofauti hii kati ya mke na hikira. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu katika mwili na katika roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyompendeza mumewe.


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu.


BASSI, kabla ya mambo yote, dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;


Mwanamume au mwanamke aamimye, akiwa na wajane, awasaidie, kanisa lisilemewe; illi liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.


Waheshimu wajane walio wajane kweli kweli.


Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,


Maana bivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumainia Mungu, wakiwatumikia waume zao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo