Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 5:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Al-Masihi Isa na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Ninakuagiza mbele za Mungu na mbele za Al-Masihi Isa na mbele za malaika wateule, shika maagizo haya pasipo ubaguzi wala upendeleo.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 5:21
25 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, twajua ya kuwa wanena yaliyo kweli na kuyafundisha, wala hujali cheo cha mtu, bali katika kweli waifundisha njia ya Mungu:


Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu.


Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena.


Nawaapisha kwa Bwana, wasomewe ndugu wote waraka huu.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo