Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 4:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru kujiepusha na vyakula ambavyo Mungu aliviumba vopokewe kwa shukrani na walio na imani na wenye kuijua sana kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuoa na pia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuoa na pia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuoa na pia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Wao huwakataza watu wasioe na kuwaagiza wajiepushe na vyakula fulani, ambavyo Mungu aliviumba ili vipokewe kwa shukrani na wale wanaoamini na kuijua kweli.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 4:3
30 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano.


Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu.


akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.


Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia.


(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru);


Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.


Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.


Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.


Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.


Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu ataharibu vyote viwili, tumbo na vyakula. Na mwili si kwa zina, hali ni kwa Bwana, nae Bwana ni kwa mwili.


Lakini, kama ukioa, huna khatiya, na bikira akiolewa, hana khatiya; lakini watu hao watakuwa na mateso katika mwili; lakini nataka kuwazuilia haya.


Lakini chakula hakituleti mbele ya Mungu; maana, tukila, hatuongezewi kitu, na tusipokula hatupunguziwi kitu.


Bassi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viuvwaji au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli.


Kwa maana killa kiumhe cha Mungu ni kizuri, waki hakuma cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani:


Bassi napenda wajane wasio wazee waolewe, wazae watoto, watawale mambo ya nyumbani, wasimpe adui nafasi ya kulaumu;


Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo