Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 4:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: Katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: Katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 4:12
19 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


MWE wafuasi wangu kama mimi nilivyo mfuasi wa Kristo.


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Ninyi mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;


na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi.


Yafahamu sana hayo nisemayo, maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.


Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.


katika mambo yote ukijionyesha kuwa namna ya matendo mema, katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahifu,


Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya mfano kwa lile kundi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo