Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 3:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 si mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna, akaanguka katika hukumu ya Shetani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya ibilisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Asiwe mtu aliyeokoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya ibilisi.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 3:6
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni.


NA mimi, ndugu, sikuweza kunena nanyi kama na watu wenye tabia za rohoni, bali kama na watu wenye tabia za mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.


NA kwa khabari ya vitu, vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna elimu. Elimu huleta majivuno, bali upendo hujenga.


Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.


Imempasa tena kushuhudiwa mazuri na watu walio nje; asitumbukie katika lawama na mtego wa Shetani.


amejivuna, nae hakufahamu neno lo lote, bali hali yake hali va ugonjwa, kwa khabari ya maswali na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya,


makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu;


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo