Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 3:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 3:3
45 Marejeleo ya Msalaba  

akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakwitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.


Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Vivi hivi mashemasi, wawe watu wa utaratibu, si wenye nia mbili, si watu wa kutumia mvinyo nyingi, wawe watu wasiotamani fedha ya aibu;


Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,


ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Msiwe na tabia ya kupenda fedha: mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.


VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?


lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo;


Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo