Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 3:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu: Alionekana katika umbo la kibinadamu, alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu, akaonekana na malaika. Alihubiriwa kati ya mataifa, aliaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho wa Mungu, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa na haki katika Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, akachukuliwa juu katika utukufu.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 3:16
81 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu.


Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.


Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake.


Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake:


Kisha Shetani akamwacha; wakaja malaika wakamtumikia.


Akawako huko jangwani siku arubaini, akijaribiwa na Shetani; nae alikuwa pamoja na nyama wakali, na malaika walikuwa wakimkhudumia.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Daud, bassi, amwita Bwana, na amekuwaje Mwana wake?


Akamtokea malaika toka mbinguni akimtia nguvu.


Ikawa wangali wakishangaa kwa haya, kumbe! watu wawili wakisimama karibu yao, wamevaa nguo za kumetameta.


Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia.


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani, na mmoja miguuni, hapo ulipowekwa mwili wa Yesu.


Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza?


Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemi; hatta konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.)


Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao;


Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na killa mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Illi upewe haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.


bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu;


Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.


(maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha kwenda kwa mataifa);


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,


na mimi pia, nipewe usemi, kwa kufumhua kinywa changu kwa ujasiri, niikhubiri siri ya Injili,


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


illi wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo,


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa.


wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Na haikanushiki kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake.


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Na katiksi kipaji cha uso wake alikuwa na jina, limeandikwa, SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAILABA NA MACHUKIZO YA INCHI.


Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya nyama amehukuae, mwenye vile vichwa saba na zile pemhe kumi.


Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo