Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 3:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AMINI neno hili, Mtu akitaka uaskofu, atamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Msemo huu ni wa kweli: Mtu anayetaka kuwa askofu, huyo anatamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Msemo huu ni wa kweli: Mtu anayetaka kuwa askofu, huyo anatamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Msemo huu ni wa kweli: mtu anayetaka kuwa askofu, huyo anatamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hili ni neno la kuaminiwa, kwamba mtu akitamani kuwa mwangalizi wa kundi la waumini, atamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hili ni neno la kuaminiwa, kwamba mtu akitamani kazi ya uangalizi, atamani kazi nzuri.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 3:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake kiwe ukiwa, wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu.


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


Neno hili ni amini, lastahili kukubaliwa na wote.


Neno hili ni neno la kuaminiwa. Maana kama tukifa pamoja nae, tutaishi pamoja nae pia;


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


Maana mtu wa kwenu asiteswe kama muuaji, au mwizi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishae na mambo ya watu wengine.


lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo