Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 2:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, kabla ya mambo yote, dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote:

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 2:1
26 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;


hatta tukamwonya Tito kuwatimilizieni neema hii kama vile alivyoianza.


Bassi naomba, msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, yaliyo utukufu kwenu.


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Namshukuru Mungu wangu killa niwakumbukapo,


Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu.


Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli.


Bali yeye aliye mjane kweli kweli, na kuachwa peke yake, amemwekea Mungu tumaini lake, nae hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.


Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,


Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo