Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 1:4
19 Marejeleo ya Msalaba  

Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


ikiwa mmesikia khabari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


Bali hadithi za kizee, zisizo za dini, uzikatae.


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;


Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.


Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi.


Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:


nao watajiepusha na kusikia yaliyo kweli watageukia hadithi za uwongo.


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


wasisikilize hadithi za Kiyahudi, na maagizo ya wana Adamn wajiepushao na kweli.


Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Maana hatukufuata hadithi zilozotungwa kwa werevu, tulipowajulislia ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa mashahidi wa ukuu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo