Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Timotheo 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aoneshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aoneshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aoneshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Al-Masihi Isa apate kuonesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Al-Masihi Isa apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele.

Tazama sura Nakili




1 Timotheo 1:16
37 Marejeleo ya Msalaba  

Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Peponi.


Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo.


lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.


Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu ana uzima wa milele; mimi nitamfufua siku ya mwisho.


na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.


Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.


KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;


illi sisi tuwe sifa ya utukufu wake, tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu;


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.


Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa;


Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo