Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 5:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 mpingeni, mkiwa imara katika imani, mkijua ya kuwa mateso yaleyale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.

Tazama sura Nakili




1 Petro 5:9
24 Marejeleo ya Msalaba  

lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.


wala msimpe nafasi Shetani.


zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.


Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.


mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.


Fanya vita vile vizuri vya imani, shika uzima wa milele ulioitiwa, ukayaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.


Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.


Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, waliziba makanwa ya simba,


Bassi kama mkiwa hamna kurudiwa walikoshiriki wote, mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.


Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.


Mnafurahi sana kwa ajili yake, ijapokuwa sasa kwa kitambo, ikiwa ni lazima, mmchuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali,


Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo