Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 5:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza.

Tazama sura Nakili




1 Petro 5:8
61 Marejeleo ya Msalaba  

na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.


Kesheni bassi: kwa maana hamwijui saa atakayokuja Bwana wenu.


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


NDIPO Yesu alipopandishwa na Roho hatta jangwani, illi ajaribiwe na Shetani.


Kisha Shetani akamwacha; wakaja malaika wakamtumikia.


Hawa ndio walio njiani, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, marra huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.


Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Bwana akasema, Simon, Simon, tazama, Shetani amewataka ninyi awapepete kama nganu:


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake.


wala msimpe nafasi Shetani.


Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani.


Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.


Na vivyo hivyo wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisetiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi, si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;


Vivi hivi wanawake wawe watu wa utaratibu, si wasingiziaji, watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.


Bassi imempasa askofu kuwa mtu asiyelaumiwa, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, mfundishaji;


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake;


yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ua kuishi kwa kiasi, na haki, na utawa, katika ulimwengu wa sasa,


ya kama wazee wawe wenye kujimudu nafsi zao, wenye adahu, wenye kiasi, wazima katika imani na katika upendo na katika uvumilivu.


illi wawatie akili wanawake vijana wawapende wanme zao, ka kuwapenda watoto wao,


Na vijana vivyo hivyo nwaonye kuwa na kiasi;


Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku.


Kwa hiyo shangilieni, mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa inchi na bahari: kwa maana yule msingiziaji ameshuka kwao mwenye hasira nyingi, akijua ya kuwa ana wakati si mwingi.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo