Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 5:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kwa msaada wa Silvano, ninayemhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kwa msaada wa Silvano, ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mwenyezi Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.

Tazama sura Nakili




1 Petro 5:12
24 Marejeleo ya Msalaba  

Petro akimwona huyu, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,


Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote;


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;


pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku.


PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


PAOLO, Silwano, na Timotheo kwa kanisa la Wathessaloniki lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo:


Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache.


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.


walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu:


Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.


Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo