Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 4:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Wao hushangaa kwamba ninyi hamjiingizi pamoja nao katika maisha yao ya uovu uliopita kiasi, nao huwatukana ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Wao hushangaa kwamba ninyi hamjiingizi pamoja nao katika huo wingi wa maisha ya ufisadi, nao huwatukana ninyi.

Tazama sura Nakili




1 Petro 4:4
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi.


Hatta baada ya siku si nyingi yule mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda inchi ya mbali: akatapanya huko mali zake kwa maisha ya uasharati.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.


Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;


Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni.


Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo