Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 4:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda wayapendayo mataifa, kuenenda katika uasharati, ua tamaa, na ulevi, ua karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kwa maana wakati uliopita, mmetumia muda mwingi mkifanya yale wapagani hupenda kutenda: wakiishi katika uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulafi, vileo, ngoma mbaya, na ibada chukizo za sanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Maana wakati uliopita mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu mkifanya yale ambayo wapagani hupenda kutenda: wakiishi katika uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulafi, vileo, ngoma mbaya, na ibada chukizo za sanamu.

Tazama sura Nakili




1 Petro 4:3
30 Marejeleo ya Msalaba  

wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.


Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.


Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,


husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu;


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu;


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo