Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 4:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa nanyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa nanyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa nanyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mkitukanwa kwa ajili ya jina la Al-Masihi, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kama mkitukanwa kwa ajili ya jina la Al-Masihi, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mwenyezi Mungu anakaa juu yenu.

Tazama sura Nakili




1 Petro 4:14
37 Marejeleo ya Msalaba  

M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu.


Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.


Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka.


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Bassi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake mtu yule; sisi tu wanafunzi wa Musa.


Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, illi uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu.


Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku.


Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.


Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.


Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo