Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 4:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote anayehudumu hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kupitia kwa Isa Al-Masihi. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mwenyezi Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Isa Al-Masihi. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.

Tazama sura Nakili




1 Petro 4:11
47 Marejeleo ya Msalaba  

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Bassi huyo alipokwisha kutoka, Yesu akanena, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, na Mungu ametukuzwa ndani yake:


Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.


Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.


Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


Pana tofauti za karama; bali Roho yule yule.


Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.


Maana mlinunuliwa kwa thamani. Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.


na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari,


Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


Ndugu zangu, mwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


killa ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.


Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.


bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima,


Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


Mtu akidhani ya kuwa ana dini, nae hazuii ulimi wake kwa khatamu, akijidanganya moyo wake, dini yake mtu yule haifai.


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.


Uweza una yeye hatta milele na milele. Amin.


Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo