Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 3:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




1 Petro 3:4
40 Marejeleo ya Msalaba  

Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu;


Mwambieni binti Sayuni, Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, amepanda punda, Na mwana punda, mtoto wa punda.


Ewe Farisayo kipofu, takasa kwanza ndani ya kikombe na chungu, illi nje yake nayo ipate kuwa safi.


Wa kheri wenye upole: maana hawo watairithi inchi.


Enyi wapumbavu, yeye aliyekifauya cha nje, siye aliyekifanya cha ndani naebo?


Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.


wakaubadili utukufu wa Mungu asiye ua uharibifu kwa mfano wa sura ya bin-Adamu aliye ua uharibifu, na ya nyama wenye mbawa, na ya nyama wenye miguu mine, na ya nyama watambaao.


hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


Kwa maana naifurahia sharia ya Mungu kwa mtu wa ndani,


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku.


upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia.


kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;


Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,


Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.


tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe kama tulivyowaagiza;


Bassi twawaagiza, hao na kuwaonya katika Bwana wetu Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.


kwa ajili ya wafalme, na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya ntulivu na amani, katika utawa wote, na ustahifu.


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, kapokeeni kwa upole neno lililopandwa, liwezalo kuokoa roho zenu.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo