Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 3:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 roho ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Nuhu, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mwenyezi Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Nuhu, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika.

Tazama sura Nakili




1 Petro 3:20
28 Marejeleo ya Msalaba  

Bali njia ni nyembamba iendayo hatta uzima, na mlango wake ni mwembamba: nao waionao ni wachache.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


mkiupokea mwisho wa imani yenu, wokofu wa roho zenu.


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


Kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni,


Bassi wao wateswao apendavyo Mungu na wamwekee roho zao kama amana, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.


wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasiomeha Mungu,


Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo