Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 3:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa kuwa Al-Masihi naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa kuwa Al-Masihi naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho.

Tazama sura Nakili




1 Petro 3:18
34 Marejeleo ya Msalaba  

Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;


Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.


Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Katika yeye tuna ajasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya imani yake.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Mmemhukumu mwenye haki mkamwua: nae hashindani nanyi.


Kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni,


BASSI kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake kwa ajili yenu, ninyi nanyi jivikeni nia ile ile kama silaha; kwa maana yeye allyeteswa katika mwili, ameachana na dhambi;


Maana kwa ajili hiyo na wao waliokufa walikhubiriwa Injili, illi waluikumiwe katika mwili wahukumiwavyo wana Adamu; bali wawe hayi katika roho kwa kumtii Mungu.


Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo