Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Bali mtukuzeni Al-Masihi kama Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Bali mtakaseni Al-Masihi kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima,

Tazama sura Nakili




1 Petro 3:15
34 Marejeleo ya Msalaba  

Paolo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usio mnyonge. Nakuomba, nipe rukhusa niseme na wenyeji hawa.


Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,


Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;


wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa khofu.


bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo