Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 3:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ajiepushe na uovu, atende mema, atafute amani na kuizingatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ajiepushe na uovu, atende mema, atafute amani na kuizingatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ajiepushe na uovu, atende mema, atafute amani na kuizingatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

Tazama sura Nakili




1 Petro 3:11
37 Marejeleo ya Msalaba  

illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Wa kheri wasuluhishi: maana hawo watakwitwa wana wa Mungu.


Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na killa mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.


Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani.


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Yesu akawaambia, Nitawaulizeni neno moja. Ni halali siku ya Sabato kutenda mema au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua?


Siombi uwatoe katika ulimwengu, hali uwalinde na yule mwovu.


Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote.


Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.


Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.


Bassi nimeona sharia hii ya kuwa nipendapo kutenda lililo jema, liapo lililo baya ni karibu nami.


Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.


watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo,


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi.


Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombo yao: Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.


Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo