Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Haya yamewajia ili imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo ingawa inasafishwa kwa moto, ionekane kuwa halisi, na imalizie kwa sifa, utukufu na heshima Isa Al-Masihi atakapodhihirishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Isa Al-Masihi atadhihirishwa.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:7
53 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Kadhalika itakuwa katika siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?


Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.


bali utukufu na heshima na amani kwa killa mtu atendae mema, Myahudi kwanza na Myunani pia;


hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi siku ile watakayofunuliwa wanawa Mungu.


kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,


Bassi, thamani hii ni kwenu ninyi mnaoamini, bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni;


Wapenzi, msione kuwa ni ajahu ule msiba unaowapata kama moto illi mjaribiwe, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho;


lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.


NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo