Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Mnafurahi sana kwa ajili yake, ijapokuwa sasa kwa kitambo, ikiwa ni lazima, mmchuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Katika haya yote mnafurahi sana, ijapokuwa kwa muda mfupi sasa mmehuzunishwa kwa majaribu ya aina nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:6
47 Marejeleo ya Msalaba  

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo nami nitawapumzisha.


Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika, na kuhuzunika moyo.


Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.


Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu.


Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.


Malaika akawaambia, Msifanye khofu; kwa maana nawaletea ninyi khabari njema za furaha kuu, itakayokuwa kwa watu wote:


Bassi na ninyi sasa hivi mna huzuni; lakini nitawaona tena, na moyo wenu utafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleae.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu;


Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.


Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi;


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Kwa kuwa alikuwa na shanku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Furahini katika Bwana siku zote; marra ya pili nasema, Furahini.


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa;


Jihuzunisheni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu kugeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa hamu.


Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo