Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Bali Neno la Bwana hudumu hatta milele. Na neno bilo ni neno lile jema lililokhubiriwa kwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.” Neno hilo ni hiyo Habari Njema mliyohubiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.” Neno hilo ni hiyo Habari Njema mliyohubiriwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.” Neno hilo ni hiyo Habari Njema mliyohubiriwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 lakini neno la Mwenyezi Mungu ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 lakini neno la Mwenyezi Mungu ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:25
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.


Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na inchi vitoweke kuliko nukta moja ya torati itanguke.


MWANZO alikuwako Neno, nae Neno alikuwako kwa Mungu, nae Neno alikuwa Mungu.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa.


akaja, akakhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na kwao waliokuwa karibu.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu:


na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.


ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Nikaona malaika niwingine akiruka kati kati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awakhubiri wakaao juu ya inchi na killa taifa na kabila na lugha na jamaa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo