Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kwa njia yake, mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kwa njia yake, mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kwa njia yake, mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kupitia kwake mmemwamini Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kupitia kwake mmemwamini Mwenyezi Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu na akampa utukufu, ili imani yenu na tumaini lenu ziwe kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:21
34 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia.


Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka.


MSIFADHAIKE mioyo yenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe;


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


kwa sababu, ukimkiri Kristo Yesu kwa kinywa chako, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua, utaokoka;


bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu,


Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Belial? Au aammiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini? Tena pana mapatano gani ya hekalu ya Mungu na sanama?


Kwa sababu hiyo na mimi, tangu nilipopata khabari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.


KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo