Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Walijaribu kujua ni wakati upi na ni mazingira yapi ambayo Roho wa Al-Masihi, aliyekuwa ndani yao, alionesha alipotabiri mateso ya Al-Masihi na utukufu ambao ungefuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Al-Masihi aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Al-Masihi na utukufu ule ambao ungefuata.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:11
29 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Maneno hayo aliyasema Isaya alipouona utukufu wake, akataja khabari zake.


Walipofika kukabili Musia, wakajaribu kwenda Bithunia, lakini Roho ya Yesu hakuwapa rukhusa,


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.


Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo