Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Petro 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Petro, mtume wa Isa Al-Masihi. Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, jimbo la Asia, na Bithinia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Petro, mtume wa Isa Al-Masihi: Kwa wateule wa Mwenyezi Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia.

Tazama sura Nakili




1 Petro 1:1
34 Marejeleo ya Msalaba  

Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake;


Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile.


Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi.


Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.


wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.


Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani?


Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.


Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilikhubiri neno.


Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao.


Maana hatupendi, ndugu, msijue khabari ya shidda ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hatta tukakata tamaa ya kuishi.


na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,


kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.


Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,


Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo