Zaburi 93 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCUkuu wa enzi ya Mungu 1 BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; 2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele. 3 Ee BWANA, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake. 4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu. 5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee BWANA, milele na milele. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya