Zaburi 82 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCOmbi la kupata haki Zaburi ya Asafu. 1 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. 2 Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya? 3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara; 4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu. 5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. 6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote. 7 Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu. 8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana mataifa yote ni yako. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya