Zaburi 70 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCSala ya ukombozi kutoka kwa adui Kwa mwimbishaji. Ya Daudi, kama matoleo ya ukumbusho. 1 Ee Mungu, uniokoe, Ee BWANA, unisaidie hima. 2 Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. 3 Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe! 4 Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. 5 Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee BWANA, usikawie. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya