Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Zaburi 65 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Shukrani kwa mavuno mengi Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.

1 Ee Mungu, wastahili sifa katika Sayuni, Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.

2 Wewe usikiaye maombi, Wote wenye mwili watakujia.

3 Tutakapozidiwa na matendo maovu Wewe utatuondolea uovu wetu.

4 Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako.

5 Kwa mambo ya kutisha utatujibu, Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu. Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia, Na la bahari iliyo mbali sana,

6 Milima waiweka imara kwa nguvu zako, Huku ukijifunga uweza kama mshipi.

7 Watuliza kuvuma kwa bahari, Kuvuma kwa mawimbi yake, Na ghasia za watu;

8 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.

9 Umeijia nchi na kuisitawisha, Umeitajirisha sana; Mto wa Mungu umejaa maji; Wawapa watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.

10 Matuta yake wayajaza maji; Wapasawazisha palipoinuka, Wailainisha nchi kwa manyunyu; Waibariki mimea yake.

11 Umeuvika mwaka taji la wema wako; Mapito yako yadondoza unono.

12 Huyadondokea malisho ya nyikani, Na vilima vimejawa na furaha.

13 Na malisho yamejawa na kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo