Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Zaburi 53 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Kushutumiwa kwa wasiomwamini Mungu Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi.

1 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.

3 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.

4 Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU.

5 Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.

6 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo