Zaburi 47 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCUtawala wa Mungu juu ya mataifa Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi. 1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. 2 Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. 3 Amewatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. 4 Ametuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ampendaye. 5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, BWANA kwa sauti ya baragumu. 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; Imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa. 7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa zaburi. 8 Mungu ayatawala mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. 9 Wakuu wa watu wamekusanyika, Kama watu wa Mungu wa Abrahamu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya