Zaburi 3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCMwamini Mungu katika dhiki Zaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu. 1 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, 2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. 3 Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. 4 Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. 5 Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. 6 Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu, Waliojipanga Juu yangu pande zote. 7 BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. 8 Wokovu ni wa BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya