Zaburi 149 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCSifa kwa wema wa Mungu kwa Israeli 1 Haleluya. Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. 2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa sauti tamu ya matari na kinubi. 4 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. 5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. 6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao. 7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya makabila ya watu. 8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma. 9 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya