Zaburi 142 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCSala ya ukombozi kutoka kwa watesi Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Ombi. 1 Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua. 2 Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. 3 Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. 4 Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. 5 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. 6 Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. 7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya