Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Zaburi 141 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC


Sala ya kutaka kulindwa kutoka kwenye uovu

1 Ee BWANA, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.

6 Wakuu wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.

7 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.

8 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga.

9 Unilinde kutoka kwa mtego walionitegea, Na kutoka kwa matanzi ya watendao maovu.

10 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Wakati ninapopita salama.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo