Zaburi 14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCKushutumiwa kwa wasiomwamini Mungu Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. 2 Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. 3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. 4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA. 5 Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. 6 Mnaiharibu mipango ya mtu mnyonge, Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake. 7 Laiti wokovu wa Israeli ungetoka katika Sayuni! BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya