1 Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA.
2 Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi BWANA.
3 BWANA akubariki toka Sayuni, Aliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.