Zaburi 131 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCKumtumainia Mungu kwa utulivu Wimbo wa kupanda mlima. 1 BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu. 2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya Kifuani mwa mama yake; Roho yangu ni kama mtoto, Aliyeachishwa kunyonya. 3 Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya