Zaburi 13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCSala ya ukombozi kutoka kwa adui Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele? Hadi lini utanificha uso wako? 2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini? 3 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti. 4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa. 5 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. 6 Naam, nitamwimbia BWANA, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya