Zaburi 129 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCSala ya kushindwa kwa adui za Israeli Wimbo wa Kupanda mlima 1 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, 2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. 3 Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. 4 BWANA ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. 5 Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. 6 Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. 7 Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. 8 Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la BWANA. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya