Zaburi 128 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCNyumba ya mwumini yenye furaha Wimbo wa kupanda mlima. 1 Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake. 2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. 3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. 4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA. 5 BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; 6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya