Zaburi 126 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCMavuno ya shangwe Wimbo wa kupanda mlima. 1 BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. 2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu. 3 BWANA alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. 4 Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. 5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. 6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya