Zaburi 125 - Swahili Revised Union Version - SRUVDCUsalama wa watu wa Mungu Wimbo wa kupanda mlima. 1 Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautikisiki, wakaa milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. 3 Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. 4 Ee BWANA, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. 5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya